MBEYA watwaa Ubingwa TAIFA CUP 2011....

Saturday, May 28, 2011 0 Comments




Timu ya mkoa wa MBEYA "Mapinduzi Starz" imetwaa kombe la TAIFA CUP 2011 kwa kuifunga timu ya Mwanza Heroes bao 1 bila majibu, goli lililofungwa na Gaudience Mwaikimba japo kabla ya mpira huo kuingia kimyani mpira uligonga mkononi mwa mfungaji bila mwamuzi kuona.

Michezo ilifanyikia jijini Arusha, ambapo timu ya mbeya imejinyakulia Kombe na kitita cha Tshs. milioni arobaini 40,000,000/= na mfungaji bora G. Mwaikimba amezawadiwa kiatu cha dhahabu pamoja na kitita cha Tshs. 2.5 milioni

Mshindi wa tatu ktk michuano hiyo wamechukua ILALA, ya pili wamechukua MWANZA..... wakati kocha bora na mchezaji bora zimekwenda Mbeya pia


Michuano imemalizika muda mfupi uliopita....HONGERA MKOA WA MBEYA - TANZANIA

Homa za wapenzi wa soka zinaelekea kwenye fainali za UEFA leo kati ya Barcelona na Man UTD

0 comments: