JAHAZI kutoka na album ya 6 Julai 30, PTA

Wednesday, July 21, 2010 5 Comments


Jahazi Morden Taarab wanatarajia kuzindua albamu yao ya sita ya My Valentine Julai 30, mwaka huu katika Ukumbi wa PTA, DSM


Mkurugenzi wa kundi hilo Mzee Yusuph amesema albamu hiyo ina nyimbo sita na katika uzinduzi huo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa mwimbaji mkongwe wa taarabu nchini, Kidude Baraka aka 'Bi Kidude' na kundi la burudani la Baikoko kutoka Tanga.


Mzee amesema pia watatambulisha wimbo mpya wa Khadija Yusuph, aliyeuimba baada ya kurudi kwenye kundi hilo wa Nilijua mtasema ikiwa ni pamoja na wimbo wa Wagombanao ndiyo wapatanao.

Nyimbo zilizopo katika albamu hiyo ni My Valentine, Langu rohoni, Wema hazina kwa Mungu, Mfamaji, Jaala haikimbiliki na Asilimia 100.


Albamu za kundi zilizotangulia ni VIP, Daktari wa mapenzi, Two in One, Tunakula kwa nakshi na Undugu hazina yetu

5 comments:

  1. hongera nduguyangu nime enjoy kutembelea blog yako karibusana wadau tupo




    Amina Zangira

    ReplyDelete
  2. This comment has been removed by the author.

    ReplyDelete
  3. jahaz wako juu sana

    ReplyDelete
  4. hi dida, so cute ,so lovely

    by the way naienjoy sana kipindi chenu cha mimitkicko ya pwani
    namo ni mdau kwa sana tuuuuuuuuuuuuuu!

    keep it up baby

    stay blessed.

    ReplyDelete
  5. unajitahidi dida lakini punguza kuonyesha sebule yako jitahidi kuweka vitu vingine vinavyoendelea katika jamii husika

    ReplyDelete