FAMILIA YA LADY JAY DEE WALIPOTEMBELEA KITUO CHA WATOTO YATIMA CHA MAUNGA - KINONDONI
Lady Jay Dee akipokea risala kutoka kwa mtoto Khadija Mussa.
Lady
Jay Dee akikabidhi msaada uliotolewa na Familia yake vikiwemo Mchele,
Maharage, Mafuta ya Kupikia, Sabuni za Kufulia, Nguo, Juisi pamoja na
vingine vingi. Anayepokea msaada huo ni Mlezi wa Kituo hicho Bi.
Zainabu Bakari (kushoto) pamoja na mmoja wa watoto wanaolelewa katika
kituo hicho Khadija Mussa.
Jay
Dee Family inawakaribisha wadau wote watakaoguswa kutoa mchango
chcochote walichonacho kupitia Jay Dee Family. Kwa mawasiliano zaidi
wasiliana na Judyjaydee@yahoo.com.
RISALA FUPI KWA MGENI RASMI - KUTOKA MAUNGA CENTRE
Ndugu Mgeni Rasmi
Maunga Centre ni kituo cha kulelea watoto yatima na waishio katika mazingira magumu.
Kituo kimeanzishwa mwaka 2008 na kusajiliwa mwaka 2011
Kituo kina watoto 50, kati yao 30 wanaishi hapa kituoni na 20 wanaishi na walezi wao.
Lakini mahitaji ya kibinadamu wanayoyapata hapa kituoni, Sisi kama
viongozi wa Maunga Centre hatupendi watoto hawa kuishi na walezi wao,
ikizingatia kuwa hawana uwezo ila kutokana na uchache wa Vyumba
imelazimika iwe hivyo.
Uongozi wa Maunga Centre unatoa shukrani za dhati kwa kukubali wito
wetu wa kuja kuwatembelea na hii inaonyesha jinsi gani unavyopenda jamii
bila ubaguzi.
Maunga Centre ilituma barua kwako ya maombi ya kuwatembelea watoto
hawa yatima ambao hawakupenda kukosa wazazi wao. Tulituma maombi kwako
kwasababu tuna imani kubwa kuwa wewe ni kioo cha jamii na mpenda jamii
bila ubaguzi wa rangi, dini, jinsia, wala ukabila wewe ni mtu wa watu
wote.
Kitendo ambacho leo umekifanya cha kuwatembelea watoto na kula nao
chakula pamoja ni kitendo cha kihistoria kwa jamii ya Watanzania na
tunaamini umefuata maagizo ya Mungu kwa dini zote.
Tukumbuke kuwa tendo la kuwatembelea yatima, kuwasaidia, kuwafariji
kwa kuondokewa na wazazi wao ni ibada au sala kubwa sana kwa Mungu
Tunawashukuru wote ambao umeungana nao katika msafara wako sisi kama
kituo tunasema hatuna cha kuwalipa ila malipo mtayapata kwa Mungu, pia
tunawaombea Mungu awape uzima, kipato na awapandishe vyeo uko kazini
kwenu ili kipato kiongezeke muweze kusaidia jamii hususani yatima.
Maunga Centre inatoa shukrani kwa misaada ambayo mmetuletea. Kituo
cha Maunga Centre kinawaomba MR.&MRD GARDNER kuwa walezi wa kituo
hiki,
Tunawaomba kuwa walezi kwakuwa tunaamini kitendo ambacho leo
mmekifanya inaonyesha jinsi gani mlivyokuwa na uchungu na swala zima la
yatima.
Tunaamini kuwa kutoa ni moyo na wala si utajiri kwasababu wapo wenye
uwezo mkubwa lakini hawajitoi kusaidia jamii kama ulivyofanya leo.
MAUNGA CENTRE ina changamoto zifuatazo:
1. Kukosa fedha za kuwalipa wahudumu
2. Kukosa eneo kubwa la kujenga kituo
3. Kukosa wafadhili
4. Watoto hawana sare za shule
5. Kukosa gharama za kuwasomesha (michango ya shule)
Tafadhali tunakuomba ututafutie wafadhili wa ndani na nje ya nchi ili
tuwasaidie na tuna imani kubwa kuwa unawafahamu watu ambao wana moyo wa
kutusaidia wa ndani na nje ya nchi.
Tunakuomba utusaidie kukitangaza kituo katika vyombo vya habari ili watu wenye moyo watusaidie.
Sisi kama kituo hatuna uwezo wa fedha za kugharamia gharama za matangazo.
Ndugu mgeni rasmi tunakuomba tamasha moja la muziki la kuchangia
fedha kwaajili ya kituo cha watoto yatima. Tunakuomba malipo utayapata
kwa Mungu.
Mwisho tunakutakia maisha mema, Mungu akupe roho ya imani pamoja na
kipato kiongezeke zaidi akupe kizazi chema ambacho kitajali jamii kama
ulivyo wewe mwenyewe
Ahsante
Karibu tena Maunga Centre
BINAFSI NINGEPENDA KUANZA NA KUWATAFUTIA KIWANJA KIKUBWA KWAAJILI YA
KUJENGA KITUO KINGINE. WAHAME HAPO WALIPO, WANABANANA SANA NA NI VYMBA
VIWILI TU AMBAVYO VINA HALI MBAYA SANA.
AKITOKEA MTU WA KUTUSAIDIA KIWANJA, TUTACHANGISHA FEDHA ZA KUANZA UJENZI:
Mimi kama JAYDEE natoa wito kwa yoyote mwenye moyo kuungana nami katika swala hili.
Ikiwa mimi na Gardner tumeombwa kuwa walezi wa kituo hicho, Pamoja tunaweza
Natanguliza shukrani:
JIDE
Watoto wako 30 na vyumba viko 2
Sasa fikiria ni wastani wa watoto 15 katika kila chumbaHakuna mtu yoyote ambae angependa kuishi katika mazingira ya namna hii, huruma ndio inayohitajika hapa
Hili ndio eneo wanalotumia kama jiko la kupikia chakula
Na hii ndio sehemu ya kujisaidia "CHOO"
Fungua moyo wako, tafadhali i beg you pipo
Haya sio maisha watoto wetu wanayostahili kukulia
Tusaidiane kujikwamua katika umasikini ili hata wakienda shule waweze kufikiria masomo na kufanya vema
Msafara ulianzia Nyumbani Lounge ambapo LA
FAMILLE tulikutana na kila mmoja alileta kidogo alichonacho ili
kuchangia watoto wa kituo cha MAUNGA
Sehemu wanayoishi watoto hao wenye ni sehemu ambayo mazingira yake sio ya kuridhsha kabisa
Kwa mtu yoyote akifika hatasita kutokwa na machozi
Hii ni njia ya uchochoro ambayo inaelekea kituoni hapo
Gari haiwezi kupita hivyo ilitulazimu kupaki barabarani na kutembea kuelekea kituoni, kama inavyoonekana kwenye picha
Huyu mama ndio mlezi wa kituo hicho
Pamoja na hali duni iliopo kituo hicho walijitahidi kupamba na kutuandalia mazingira tujisikie kama wageni
Watoto wengi ni wenye umri mdogo sana ambao wanahitaji malezi na uangalizi wa hali ya juu
Beautifull
GK akisaidia kushusha vyakula vya msaada kituoni hapo
Nyumba wanamolala watoto hali yake si nzuri hata kidogo
Vitanda ni vichache kwahiyo huwalazimu kubanana
Happy Happy
Wanty
Maggie Musa na Leon Lee
Sab
Wise Monica Kaaya
Tulijikuna mpaka hapa japo kuna mengi wanayoyahitaji zaidi
Faraji
Binti alisoma risala ilioelezea matatizo wanayokumbana nayo kituoni hapo
Sisi kama LA FAMILLE hatukwenda kituoni hapo kwaajili ya show off
bali waliniandikia barua ya kuomba msaada nami nikaona ni vema
kusaidiana na wenzangu.
Na wanahitaji kutangaziwa zaidi ili watu wengi wajitokeze kusaidia kwani hali yao ni tete ki fedha na kimahitaji
Nili play part yangu mpaka hapa ila kwa bahati mbaya nasikitika kuwa
sikuweza kukaa muda mrefu na kula chakula cha mchana pamoja na watoto
hao kutokana na kuwa ilinibidi niwahi airport kuelekea BUNDA kwa mazishi
ya bibi yangu.
Ila mimi pamoja na staff wa NYUMBANI LOUNGE tuliandaa chakula na niliacha LA FAMILLE waniwakilishe kwa ratiba iliobakia
PICHA ZOTE NA MAELEZO YANAYOFUATA KUANZIA HAPA NI KWA HISANI YA ZAINUL MZIGE WA MO DEWJI BLOG
Lady Jay Dee na baadhi ya wanafamilia wakipiga makofi baada ya risala kusomwa na mtoto Khadija Mussa (hayupo pichani).
Lady Jay Dee akipokea risala kutoka kwa mtoto Khadija Mussa.
Lady
Jay Dee akikabidhi msaada uliotolewa na Familia yake vikiwemo Mchele,
Maharage, Mafuta ya Kupikia, Sabuni za Kufulia, Nguo, Juisi pamoja na
vingine vingi. Anayepokea msaada huo ni Mlezi wa Kituo hicho Bi.
Zainabu Bakari (kushoto) pamoja na mmoja wa watoto wanaolelewa katika
kituo hicho Khadija Mussa.
Jay
Dee Family inawakaribisha wadau wote watakaoguswa kutoa mchango
chcochote walichonacho kupitia Jay Dee Family. Kwa mawasiliano zaidi
wasiliana na Judyjaydee@yahoo.com.
Lady Jay Dee akibadilishana mawazo na walezi wa kituo hicho baada ya kukabidhi msaaada huo.
Mwanafamilia Ester Ulaya (kushoto) akiteta jambo na Komando Binti Machozi Lady Jay Dee.
Pichani
Juu na Chini Wanafamilia wa Lady Jay Dee wakipakua chakula
kilichoandaliwa Nyumbani Lounge kwa ajili ya kula pamoja na watoto
yatima wa kituo cha Maunga Centre.
Watoto wa kituo cha Maunga Centre wakipata chakula cha mchana kilichoandaliwa na Jay Dee Family.
Vijana wa Jay Dee Family wakiwajibika kuhudumia chakula kwa kituo cha kulelea watoto yatima cha Maunga Centre.
Mlezi
wa kituo cha Maunga Centre Bi Zainabu Bakari ambapo amezungumzia
changamoto zinazowakabili ni sehemu ya kuishi wahudumu wa kituo hicho,
mishahara ya kuwalipa wahudumu na makazi ya wahudumu wa kituo hicho.
Bi.
Zuhuru Bakari alisema kituo hicho kinalea watoto 30 ambapo watoto 20
wanalelewa nje ya kituo kwa baadhi ya walezi waliowachagua wao kutokana
na ufinyu wa eneo jumla yake inatengeneza idadi ya watoto 50.
Mwanafamilia
Ester Ulaya akizungumza kwa niaba ya Jay Dee Family ambapo amesema
watakuwa bega kwa bega na kituo hicho na kuendelea kuwatafutia wafadhili
wa kusaidia kituo hicho.
Baadhi ya wanafamilia katika pozi na walezi wa kituo hicho.
Wanafamilia katika picha ya pamoja na walezi wa kituo hicho pamoja na watoto yatima wanaolelewa kwenye kituo hicho.
Zainul Mzige wa MO BLOG alijumuika na Familia ya Jay Dee katika kutoa msaada kwa watoto yatima wa kituo cha Maunga Centre.
0 comments: