HI HATERS.

Tuesday, September 28, 2010 26 Comments

Nawapa pole sana wale mnaonichukia ila ukweli utabaki pale pale mmefunga banda wakati farasi kesha toka,na mjue tu ya kwamba hakuna nyumba inayokosa ukumbi nawatakia maisha marefu myaone yangu mengi na bado huo mwanzo nitastirika kwa nguvu za manani sili cha mtu na wala sitegemei cha mtu mtabaki mnalalo hampati mtakalo yangu yananienda acheni nijishaue na nyie uwanja wenu.nimezaliwa kwa bakti sijui nyie maheters mlozaliwa kwa bahati mbaya.mtasema mchana na msichoke kuniandama sibadili msimamo wangu.mchana mtanisema usiku mtalala wenzangu siogopi,sishtuki,hamnikoseshi raha mjini,sipati vidonda vya tumbo kwa kuwawazia nyie mashoko mzoba, najua waja wazito kama unga wa dengu na wagumu kama ngozi ya futi cha mwisho mkielewe tu mie kama shimo la taka msichoke kutupia uchafu wenu mtapiga kimya mwisho wa siku mtabaki sura ndogo kama nukta poleni kwa ukavu kama jiwe la jangwani mahers karibuni mmeamsha shetani langu makata msubiri kumpunga.

26 comments:

  1. Dadangu pole sana na yaliyokukuta, wanaochonga hawajui dunia hapa tambala bovu na tunapita tu. Yakwao mengi wameyafunika lakini moyoni hawana amani naamini utasimama imara siku si nyingi, make wewe u mpiganaji.

    ReplyDelete
  2. Werawera saafisana mamito nimeipenda hiyooooooo chezea wewe na kama mtu anaweza nae si ajishaue,kujishaua hakulipiwi VAT babu wee kamua mama songa mbele achana nao hawana lolote MASIKINI WA ROHO,MATAJIRI WA ROHO MBAYA NA CHUKI ZIMEWAJAA.DIDA atabaki kuwa DIDA.uko juu mamito miaka mia nane.USIJAL LOLOTE.



    Amina Zangira

    ReplyDelete
  3. binam me hoi kwa hii style yako ya kurusha jiwe gizani, atakayesema yalaaaaaaaaaaahhhhh!!!limemkong'oli!!!!!!!!
    watajibeba kwa mbeleko ya ngoziiiiiiii!

    ReplyDelete
  4. DIDA MAMA ANGU WAPEEEEEEE!! WAMEZOEA HAO HAWANA SHUGHULI ZA KUFANYA MAFISADI KIWEMBE! KILA UFANYALO KWAO BAYA NA WATAKUFA NACHO VIJIBA VYA ROHO WEWE YULEEE ANGANI UNA PAAAAAAAAAA MAMA PIGA KIMYA HILO JIPU LA WAJINGA WAJINGA WAPOTEZEEEEEEEEEEEE!! HAPO KAZI TUU!! MAJUNGU KWAO (WEWE UNAINGIZA SIKU KAMA KAWA MWISHO WA MWEZI HUOOOOOOOO) BY S.J

    ReplyDelete
  5. Dida oooh Dadi bwana mi nina langu nilivyoona umeanzisha hii kitu kinajua nasie akina mbali tutafaidi uhondo angalu utuwekee video bibi khah! tushindwe jichana kuku hata mziki basi mie hasa mbovu mwenzio nishushie kusema siwezi mdomo wangu ndio hizo taarab bibi hasa hiko kideo, mbona watahama na mkataba haujeshaaaa!!!!

    mdau USagara a.k.a mama NJ

    ReplyDelete
  6. yanawauma nyie hamna lolote anawapa na nyie mnayenu kibao yanawachoma wala usyajali dida ndio ujue maadui wako wengi uko juuu sana kaza buti wao tomato tu hawana lolote.

    ReplyDelete
  7. wasiokupenda wapo ila wajue mwisho wa ubaya ni aibu unawapa kubwa heri uwe na maadui wanaojionyesha kwako kuliko nmtu anayejifanya anakuchekea wanawake wengi hatupendani hasa wakiona maendeleo ya watu ni mdada najiheshimu nakwambia hao ni watu wachache wanaotaka kukukatisha tamaa tu ya maisha ila komaaaa sana wewe ni mdogo sana acha wakuseme hao ni maadui wachache fanya kazii endelea na biashara zako si wote watapenda maendeleo yako.

    ReplyDelete
  8. wasichana wa tanzania wa ajabu sana hawapendani mno mwenzenu akifanya kitu hampendi kusaidiana hasa mkimuona mwenzenu anamaendeleo ila anawaaambia ukweli sijui mkoje haters wako wengi ila acheni roho za kwa nini kuwa makini tu hawakutakii maisha mazuri.

    ReplyDelete
  9. kweli nimeamini mungu akikufungulia unapata maadui wengi sana kuwa na moyo dida hayo maisha wasiokupenda wachache na wanaokupenda wengi pole ndio dunia ila usichoke wala wasikukatishe tamaa kabisa binadamu ndivyo walivyo uko juuu wanakukubali ila wanaogopa kukwambia ukweli maneno yako kuntu.

    ReplyDelete
  10. unaniuaaaa mbavu zangu dida eti mashoko mzoba blogu yako inatusaidia kufikisha ujumbe akyamungu we mtoto mungu akuweke.

    ReplyDelete
  11. wabongo mnalo kitu icho tunakupenda sana tukija bongo tutakutafuta maneno yako yanatufanya tupate faraja nchi za watu kwa wabaya wetu.

    ReplyDelete
  12. tatizo kanajishaua sana na maringo mno.

    ReplyDelete
  13. unawafunga midomo sana achana nao dida hawana lolote siku zote wameyaweka ila hawakuwezi kbs ndio maana wanaumia kaza buti

    ReplyDelete
  14. eti huyo anon anaringa ringa na wewe basi dhahiri mnajionyesha jinsi gani mlivyo na roho mbaya jamani binadamu hii dunia tu inapita waja acheni majungu nimegundua anayoyazungumza mengi yanawagusa na yanawachoma sana dida wape kiukweli siwapendi watu kama hawa wasiomtakia mtu mema ni wauwaji mno.

    ReplyDelete
  15. na ungekuwa mzuri sana tusingekunywa maji unajishaua tu huna lolote acha mashauzi na majivuna yakijinga unachamba hata kama blogu yako inahuuuuuu.

    ReplyDelete
  16. ndio hivyotena na wewe fungua ya kwako huna jipya.dida tupe swaga kwa raha zako mamito hapo ndio mwisho kiboko ya mashoko mzoba dida uko juu.

    ReplyDelete
  17. Dida wewe nadhani unahitaji mtu wa kukufanyia cancelling kidogo, hivi kwani mtu akikusema huwa unapungukiwa na nini? mdomo mali yake mwache aongee mpaka achoke, wewe mwenyewe unasemaga kwenye kipindi chako kunyamaza ni jibu la mjinga, sasa kwanini usinyamaze akawa mjinga huyo anayekuchokonoa, na kweli ungekuwa mzuri kama wakina marehemu amina chifupa sijui ingekuwaje maana mh? hii blog nadhani umeifungua kwa ajili ya kuchamba watu, embu iga mfano wa kina dina marios, shamimu zeze na wengine wengi wenye blog, sidhani kama hayo ndo matumizi yake, utafanya ipigwe marufuku kutumia blog sasa. embu nyamaza kwanza tupumzike kwanza, kila kukicha ni wewe unasemwa kwani dida mdogo wangu ni kipi hasa ulicho nacho wewe kushinda wengine? embu punguza mdomo kidogo basi dada, je kama ungekuwa hujapata hiyo nafasi ya kufanya kazi hapo times sijui hayo majungu ungeyapikia wapi dada, au ndo ungeshika mike upitekila mahali useme? kuwa muelewa unajazwa ujinga na wee ukifika kwenye kipindi unaanza kuongea, nilikuwa nakusikiliza sana kipindi chako tukiwa ofisini ila tumeacha loh unakera sana, huo ni ushauri naomba ufanyie kazi halafu utaona majibu, ni kwa nia nzuri tu. sasa unamfundisha nini mtoto wako? kwani yeye hasikilizi radio? au akiwa anacheza na watoto wenzie unafikiri anapata maneno gani? huyu mtoto ndio mama yake yule anayependa majungu radioni sio sawa,

    ReplyDelete
  18. WE Anonymous 1:55 NAKUSHANGAA SANA KAMA WEWE MZURI TUMA PICHA KWA DIDA TUKUONE HUO UZURI WAKO BASI HOVYOOOOOOOOOOOOOOOOOOOO!!!!!!UNA LOLOTE MAJUNGU TUU YAMEKUJAA UNALO HILO! KWA TAHARIFA YAKO DIDA ANABAKI KUWA DIDA YULE YULE WA. BY S.J

    ReplyDelete
  19. "Never give up, for that is just the place and time that the tide will turn" Harriet Beecher Stowe

    ReplyDelete
  20. Ndiooooooo!
    wape wape panadoli zao,
    shingo feni ma--ko kama ubao!

    ReplyDelete
  21. Dida my dear, mi sijapenda hii blog yangu unavyoitumia, kama unahisi kuna anaekutukana au anakufanyia chochote kwanini usimface ukaongea nae, unatukatisha tamaa ya kuingia kwenye blog yako. kwani tunachotegemea sio tunachokipata, YAANI NI JINSI GANI UNAONEKA MSWAHILI.

    ReplyDelete
  22. Heeee unachekesha wewe eti anaonekean mswahili kwa lipi,alikwambia yeye anataka uzungu..unalo hilo limekuchwea ama na wewe ni wale wale...Dida wape kubwa then achana nao maninah zao...hawaoni kichaka basi mimavi hinha...wewe ni Dida utabaki kuwa Dida nothing else...uko juuuuuuuu

    ReplyDelete
  23. Coment ya Sep 29,2010 1021 jua hapa ni nyundo tu hamna msalie mtume, hamna cha faida zaidi ya kupigana vijembe.

    ReplyDelete
  24. nimegundua kuna watu ndo wanamharibia dida kwa kumshabikia awe analumbana na baadhi ya watemebeleaji wa blog yake. kama alivyosema mchangiaji mmoja hapo juu, Dida, sidhani kama watu hawa wanakutakia mema. wanakushabikia useme ya kusema lakini hatimaye sidhani kama hata kama wanakujali kihivyo. nijuavyo kazi ya media ni kuelimisha, kuburudisha, kukosoa n.k. sasa hii blog yako bila wewe kujua hao wanaojiita supporters wanakuharibia. na mtu akisema wewe mswahili hamanishi kuwa yeye ni mzungu ila anachotaka kusema huna ustarabu..lazima tukubali ni usemi ambao umezoeleka kwa vile tu inadaiwa kihistoria kaba ya kuja wakoloni wenyeji tulikuwa hatujastarabika hadi warabu then wazungu walipokuja ndo tukapata ustaabu (kihistoria, i stand to be corrected) sasa malumbano hayo ya nini? Weka mada zenye akili, tujadili..blog ya mdada mwenzetu inakuwa ndo kijiwe chetu cha kuelimishana, kupeana taarifa... hata wakaka watachangia. kwa staili hii ya sasa sidhani kama kuna mkaka atapoteza muda wake kutembelea tena once akishaona upuuzi huu..mana ni aibu tupu... mimi nakulaumu wewe dida kwa sababu ndo chanzo cha yote na pia unarubuniwa na hao wanaojifanya wanakusapoti kumbe wakupoteza usifanye la maana katika blog yako! nakuomba Dida, jaribu kubadilika.Kutembelea blog yako ni jambo la sifa, sasa nashangaa unawaiga hao washabiki eti kama mtu hataki asitembele blog hii...ni upuuzi kusema hivi..kwani watu hutembelea blog wapate kujifunza, kuburidika na hata kutoa maoni yao juu ya jambo flani.ziko blog nyingi sana. mtu akiwa na muda hutembelea karibu zote (namaanisha za hapa nyumbani hasa zile maarufu tuzijuazo)zote kwani kila mtu anayo style yake ya kufikisha ujumbe..na mara chache sana wanablog wakagongana katika maoni au mada kwa ujumla..hivyo ni vema ukaanza kuwa productive sasa. mana haya unayoendekeza yanakuchafulia tu. na hao supporters si chochote wanakuharibia haswa... igaa mifano ya wanawake wenzie wanaoendesha blog kama wewe tena wengine ni wanahabari kama wewe..hukuti wanaendekeza malumbano na blog visitors...kwani hawakosolewi? wanakosolewa..wanajaribu kusimama na ili uendelee unahitaji marafiki na wanaokupinga..wanaokupinga wanakupa nguva zaidi ya kusonga mbele.ALAMSIKI!!!

    ReplyDelete