MZEE NELSON MANDELA AFARIKI DUNIA

Friday, December 06, 2013 2 Comments

Rais wa zamani wa Afrika Kusini, Nelson Mandela amefariki dunia muda mfupi uliopita akiwa na umri wa miaka 95 jijini Johannesburg, Afrika Kusini. Rais wa nchi hiyo, Jacob Zuma amethibitisha taarifa hizo!
Mzee Mandela aliyekuwa akisumbuliwa na homa ya mapafu amefariki akiwa amezungukwa na familia yake nyumbani kwake Johannesburg.Mandela atazikwa kitaifa na bendera zitapepea nusu mlingoti alisema Rais Zuma.
Alikuwa akipatiwa matibabu kwa takribani miaka mitatu iliyopita na hali yake ilibadilika zaidi katika miezi sita ya mwisho kabla ya kifo chake.Mpiganaji huyo wa ubaguzi wa rangi, aliingia Ikulu ya Afrika Kusini akiwa mtu mweusi wa kwanza kuiongoza nchi hiyo mwaka 1994 mpaka 1999 baada ya kutumikia kifungo cha miaka 27 gerezani.Waziri Mkuu wa Uingereza, David Cameron amesema: "taa kubwa imezimika duniani.
Mungu ailaze roho ya hayati Nelson Mandela mahala pema peponi. Amina!

2 comments: