"FFU" KUPELEKA HEWANI "SUPU YA MAWE"

Tuesday, July 03, 2012 2 Comments


 
Watanzania Kushereke Saba Saba na CD " BONGO TAMBARARE"
ya Ngoma Africa Band
  
     Nyimbo za "Supu ya Mawe" na "Uhuru wa Habari" Kutinga Redioni

Wakati tunapoelekea katika shamra shamra ya sikuu ya Saba Saba,
watanzania tunafurahia sikuu hii kwa kupata burudani ya raha ya nyimbo mpya zilizopo katika CD "Bongo Tambarare" kutoka kwa bendi maarufu ya muziki wa dansi  Ngoma Africa Band aka FFU yenye maskani nchini Ujerumani, CD hiyonyimbo tatu  "Bongo Tambarare" , "Supu ya Mawe" na "Uhuru wa Habari" Inasemekana imeshaanza kupiga hodi katika milango ya vituo mbali mbali vya redio duniani na hapa nyumbani itasikika wakati wowote kuanzia sasa,hili watanzania wenye
Bongo Tambarare yawe wapate raha ya muziki.
CD hiyo yenye nyimbo tatu zilizojaa ujumbe wenye furaha na mafunzo kwa jamii, kama vile "Supu ya Mawe" ni utunzi na  wake kiongozi wa bendi hiyo kamanda Ras Makunja wa FFU akiimba kwa kushirikiana na mpiga solo afande Chris-B.
Watanzania tuipokee CD "Bongo Tambarare" na tufurahie Saba Saba kwa  kupata raha ya "Supu ya Mawe" kutoka kwa Kikosi kazi Ngoma Africa aka FFU. unaweza kusikiliza pia at www.ngoma-africa.com au http://www.ngoma-africa.com

2 comments:

  1. Ngoma Africa aka FFU muziki wenu mkubwa mnatisha

    ReplyDelete
  2. Supu ya mawe ! ngoma africa band chini ya kamanda ebrahim makunja aka mkuu wa ffu,mnatuogopesha supu ya mawe yenu tutakunywa vipi?

    ReplyDelete